Hamilton ashinda tena huko Russia |
Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton
aliibuka mshindi wa mkumbo wa Russia wa mbio za magari ya langalanga
katika shindano lililokumbwa na ajali nyingi.
Kufuatia ushindi huo
mkubwa raia huyo wa Uingereza amekaribia sasa kutawazwa mshindi wa
mwaka huu wa mbio za magari ya langalanga ubingwa wake wa tatu wa duniaHamilton alikuwa katika nafasi ya pili kuelekea dakika za mwisho mwisho za mashindano hayo kabla ya dereva mwenza wa Mercedes Nico Rosberg kukabiliwa na matatizo ya injini.
| Hamilton alikuwa katika nafasi ya pili kuelekea dakika za mwisho mwisho za mashindano hayo kabla ya dereva mwenza wa Mercedes Nico Rosberg kukabiliwa na matatizo ya injini. |
Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel alimpiku Rosberg kutoka katika nafasi ya pili katika jedwali la msimamo wa dereva bora msimu huu.
Dereva wa Force India, Sergio Perez alimaliza katika nafasi ya tatu baada ya dereva shupavu wa Ferrari, Kimi Raikkonen, kuhusika katika ajali mbaya na gari la Williams lililokuwa likiendeshwa na Valtteri Bottas katika mzunguko wa mwisho.
ALAMA 9
Hamilton ameshinda sasa mashindano 9 msimu huu na hivyo anahitaji alama 9 pekee kutawazwa bingwa mara tatu duniani.
| Hamilton ameshinda sasa mashindano 9 msimu huu |
Mashindano yajayo yatakuwa Marekani.
Licha ya kumaliza katika nafasi ya 5 Raikkonen alipata pigo alipoadhibiwa kwa kusababisha ajali na hivyo alimaliza katika nafasi ya 8.
Ushindi huu hata hivyo umeikabidhi Mercedes taji la mwaka huu la watengenezaji magari.
No comments:
Post a Comment